Nelson Mandela kwa sasa anendelea kupata nafuu nyumbani. Serikali ya
Afrika Kusini imesema atakuwa akipata huduma sawa za zile alizokuwa
akipewa hospitalini jijini Pretoria.
Maafisa wa serikali wameongezea kuwa
nyumba yake imekarabatiwa kuwezesha madakatari kumtibu akiwa humo.
Madakatri wataalam ambao wamekuwa wakimshughulikia wataendela kumtibu
nyumbani mwake, lakini ikiwa hali yake ya afya itahitaji huduma za
hospitali basi atarejeshwa humo bila kuchelewa.
Inasemekana kurudi nyumbani kwa Mandela kumetia
matumaini kwa familia yake pamoja na taifa la Afrika Kusini. Hata hivyo
Mzee Mandela bado anaonekana mwenye afya dhaifu.
Serikali ya Afrika Kusini ilisema hapo jana kuwa Mandela, alitolewa hospitali ambako amekuwa akitibiwa mapafu tangu mwezi Juni.
Taarifa katika tovuti ya rais wa Afrika Kusini
ilieleza kuwa Bwana Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwengine
inabadilika.
Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.
Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu. |
No comments:
Post a Comment