TOTOLII KIMATH
Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la 'Totolii Kimath' anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Moshi kwa kosa la kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro 'Robert Boaz' alisema mfanyabiashara huyo anamiliki maduka ya kuuza na kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitokea Dubai.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi lilikuwa likifanya uchunguzi kwa muda mrefu wa picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na simu ambazo zinaonyesha mwanaume na mwanamke wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile. Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu(penal code) kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile. Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan Whatsapp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo stendi kuu ya mabasi Moshi.
Hii saafiii Itawashikisha adabu polisi
ReplyDelete