Nguza Viking na Mwanae wakitoka Mahakamani |
Mahakama, nchini Tanzania imetupilia mbali ombI la kusikilizwa upya kwa kesi dhidi ya muimbaji Nguza
Viking, anayejulikana kama Babu Seya pamoja na mwanawe, ambao
walihukumiwa maisha jela, kwa kosa la ubakaji.
Majaji walisema kua kuna thibitisho tosha kuwa wawili hao waliwabaka watoto 10 wa shule ya msingi mwaka 2013.
Katika kesi yao ya kwanza ya rufaa
miaka mitatu iliyopita, watoto wengine wawili wa muimbaji huyo,ambao pia
walipatikana na hatia ya kosa hilo mwaka 2004, waliachiliwa.
Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa Viking katika nchi hiyo iliyo katika kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba,
ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na
ufuasi mkubwa huko.
Mwandishi wa BBC Ben Mwang'onda mjini Dar es
Salaam anasema kuwa Viking na kijana wake Johnson Nguza ambaye pia ni
mwanamuziki, walifika mahakamani kwa uamuzi huo.
Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.
Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule
ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa
katika shule ya msingi ya Mashujaa mtaani Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kua muimbaji
huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndio lilikuwa ombi
lake la mwisho.
KWA MSAADA WA BBC
Huyu jamaa wanamuonea tu
ReplyDelete