Msaniianayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa
kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa
anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata
matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.
Mwanamuziki
huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya
kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini
kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana
Ukimwi.
Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni
alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika
Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali
kwenye kanisa hilo.
“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu
kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya
Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana
watu wanatafsiri kuwa nimeokoka. By Peruzibongo blog
No comments:
Post a Comment