WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Benard Membe, amewaomba radhi wananchi wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa
kutoonekana jimboni kwake muda mrefu.Alisema hali hiyo imechangiwa na majukumu
aliyonayo kitaifa, kimataifa na kuahidi kutumia muda wa likizo kufanya ziara
katika jimbo hilo ili aweze kuzungumza na wananchi
.Bw. Membe aliyasema hayo juzi wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ili kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa
chama hicho, uliofanyika kwenye Kata ya Kiwalala, iliyopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Lindi.
A l i s e m a m a j u k u m u aliyoongezewa
serikalini, yamechangia kwa kiasi kikubwa kutofika jimboni kwake mara kwa mara
hivyo hutuia muda mwingi kutekeleza majukumu hayo."Si kwamba nafanya
makusudi, leo nimewaomba radhi lakini simaanishi kuanzia sasa muda wote
nitakuwa jimboni si kweli, nazungumza hivi ili mnielewe," alisema Bw.
Membe.
Alisema yeye ataendelea kuwapenda wapigakura wake
ambao ndio waliompa nafasi ya kuwa mbunge wao hivyo kutoonekana kwake jimboni
kusiwanyong'onyeze.Wakati sijaongezewa majukumu, nilikuwa nakuja kila mwezi
lakini hivi sasa nashindwa kufanya hivyo, nimeelemewa na mzigo mzito, baadhi
yenu mnafahamu hilo,," alisema
Chanzo: Majira
No comments:
Post a Comment