Friday, 27 September 2013
NGASSA ALIPA DENI LA MILIONI 45 KWA SIMBA LEO
Mshambuliaji hatari wa Taifa Stars na Yanga Halfan Ngassa amefanikiwa kulipa deni alilokuwa anadaiwa na timu ya simba leo.Ngassa alitinga katka ofisi za TFF mnamo majira ya jioni akiambatana na mjumbe wa secretarieti ya yanga Bwana Patrick Naggi kwenda kukabidhi Hundi ya shilingi milioni 45 kwa TFF.
Ngassa alikuwa anadaiwa na timu ya Simba millioni 45 baada ya kuvunja mkataba wake na timu hiyo,hivyo alitakiwa kurudisha pesa alizopewa alipokuwa anasaini mkataba na simba.Licha ya deni hilo Ngassa alikuwa anakabiliwa na adhabu ya kutocheza mechi 6 za ligi kuu ambapo tayari mechi hzo zimeshatimia na Kocha Brandts anatarajia kumchezesha katika mechi dhidi ya Rvuvu Shooting Jumamosi hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment