Mapema asubuhi ya jana Agosti 19 'Sheikh Ponda'
Amesomewa Mashtaka 3 kwenye Mahakama ya mkoa wa Morogoroambapo kati ya
mashitaka hayo lilikuwamo lile la uchochezi alilolitoa Kwenye Mkutano
wa Hadhara siku ya Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu
Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani
kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali '' akiwa kwenye viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.
Taarifa kutoka mahakamni hapo zinadai kuwa Upelelezi Umekamilikaa zidi ya tuhuma zinazomkabili 'Sheikh Ponda' ambapo
Dhamana Imefungwa na Amerudishwa Rumande hadi siku ya tarehe 28 mwezi
huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa
Morogoro.
No comments:
Post a Comment