Saturday 28 September 2013

JUDGE WARIOBA AKIRI SHERIA YA MABADILIKO INA MAPUNGUFU

JUDGE WARIOBA

JUDGE WARIOBA


Mwenye kiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji 'Joseph Warioba' amekiri ya kuwa sheria ya mabadiliko ya Katiba mpya ina mapungufu kutokana na sheria hiyo kueleza kuwa tume hiyo itavunjwa baada ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba, ilihali ikieleza kuwa itahusika tena kusimamia utoaji wa elimu ya kura ya maoni. Kauli hiyo ya Warioba imekuja wakati vyama vya NCCR Mageuzi, Chadema na CUF, vikifanya mikutano nchi nzima kuwashawishi wananchi kupinga kile wanachokiita hujuma dhidi ya upatikanaji wa Katiba Mpya.
Sheria hiyo ambayo 'Joseph Warioba' amesema ina upungufu, muswada wa marekebisho yake ulijadiliwa na kupitishwa na wabunge Septemba 6, mwaka huu katika Mkutano wa 12 wa Bunge Mjini Dodoma, huku wabunge wa upinzani wakisusia vikao kadhaa vya mchakato huo. Rasimu hiyo ilibadilishwa baadhi ya vifungu na hivi sasa Rais Kikwete anasubiriwa kuusaini ili iwe sheria kamili. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba alisema: “Mwisho wa kazi ya tume ni baada ya kukabidhi rasimu, hilo ni tatizo. Maana tume itakuwa imeshavunjwa, sasa itafanyaje kazi ya kutoa elimu kwenye kura ya maoni?” KWA MSAADA WA THE BRAX

1 comment: