BONGO FLEVA

MSANII DIMOND AMNUNULIA GARI MZEE NGURUMO
Katka hali inayoonesha ya kushangaza na kupongezwa ,msanii Dimond amemnunulia gari mkongwe wa muziki wa dansi nchini Muhidin Ngurumo.Dimond alisema ameguswa sana na maneno ya mzee Ngurumo alipokuwa anaaga fani ya uimbaji ambapo alibainisha kuwa tangu aanze muziki enzi za ujana wake hajawahi kumiliki gari.HONGERA SANA DIMOND
Dimond akimkabithi funguo mzee Ngurumo

Mwonekano wa gari alilonunuliwa mzee Ngurumo


                                   RAY C AKANA HANA UKIMWI NA HAJAOKOKA



Mwanamuziki anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.

Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.

 

“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka.


No comments:

Post a Comment