Wednesday 28 August 2013

MSICHANA ACHAPWA VIBOKO KWA KUVAA NGUO FUPI ARUSHA

Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la NMC jijini arusha kwa sababu ya kuvaa nguo fupi.Msichana huyo aliokolewa  wasamaria wema kwa kutumia nguvu kubwa ili kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine. Watu walio shuhudia tukio hilo wamedai kuchukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana waliamua kumwadabisha ili aache tabia hiyo.

msichana akienda kuhifadhiwa 

Kwa upande wao wanawake waliomsitili msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.

No comments:

Post a Comment