Sunday 25 August 2013

ASKARI POLISI WAFUKUZWA KAZI NA WAZIRI NCHIMBI

                                                           
                                                                 WAZIRI NCHIMBI
Waziri wa mambo ya ndani ya Tanzania 'Emmanueli Nchimbi' amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi askari polisi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi la polisi.

Waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha na Mratibu wa Polisi 'Ramadhan Giro' Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta 'Jamal Ramadhan' Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Dumila Inspekta 'Juma Mpamba' na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya 
Kasulu ASP 'Daniel Bendarugaho' na kumsimamisha kazi Inspekta 'Isaack Manoni'. 

'Ramadhan Giro' alivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maafisa walio chini yake ambao walikamatwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 540 kwa kutumia gari la polisi, Inspekta 'Jamal Ramadhan' amevuliwa madaraka yake kwa kutochukua hatua stahiki baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara wa Mvomero Samson Mwita kubambikiwa fuvu la kichwa cha binadamu na askari polisi watatu wakishirikiana na matapeli wawili, Inspekta 'Isaack Manoni' amesimamishwa kazi na atashtakiwa kijeshi kutokana na tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa, Cpl. Edward aliyekuwa dereva wa gari la Polisi lililokamatwa na bangi, Inspekta 'Juma Mpamba' amevuliwa madaraka hayo kwa kuonesha udhaifu katika utendaji wake wa kazi kwa kutosimamia kikamilifu askari walio chini yake kitendo kilichosababisha askari kujipangia kazi nje ya utaratibu na kumbambikiza mfanyabiasha huyo kesi kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi. ASP 'Daniel Bendarugaho' amevuliwa madaraka kwa kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa kesi ya mauaji ya marehemu 'Gasper Mussa Sigwavumba' aliyeuawa baada ya kupigwa na askari polisi wawili Desemba 2012.

No comments:

Post a Comment