Thursday, 7 August 2014

MUME NA MKE WAISHI PAMOJA KWA MIAKA 62 NA WAFARIKI PAMOJA WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO

Don na Maxime enzi za uhai wao huku wakiwa wamejawa na furaha


Don na Maxime wakiwa wameshikana mikono hata baada ya kufariki

Mume na mke walioishi pamoja kwa miaka 62 pamoja wameshangaza watu huko Marekani kwa kufariki siku moja huku wakiwa wameshikana mikono. Maxime ambaye ni mke na Don ambaye ni mume walipishana masaa manne tu ya vifo vyao. Maxime alikuwa mgongwa wa kansa wa siku nyingi huku mumewe alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyonga. Siku yao ya mwisho ilikuwa pale walipotolewa hospitali na ndugu zao kurudishwa nyumbani ambapo Maxime alianza kufarikina mara tu baada ya Maxime kutolewa chumbani Don alifariki dunia.Kilichoshangaza zaidi ni kwamba walifariki dunia huku wakiwa wameshikana mikono.Haya ni mapenzi ya kweli ya kufa na kuzikana.

Friday, 18 July 2014

IZZY TZ: Beyoncé - Pretty Hurts......HEBU TAZAMENI HUU WIMB...

IZZY TZ: Beyoncé - Pretty Hurts......HEBU TAZAMENI HUU WIMB...

PATA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAPA

PATA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAPA
DKT.JOYCE NDLICHAKO.Katibu mtendaji baraza la mitihani

Baraza la mitihani la taifa limetangaza matokeo ya Watahiniwa wa Kidato cha 6,kama ulifanya mtihani wa kidato cha 6 mwaka huu 2014

.http://www.necta.go.tz/matokeo2014/ACSEE.htm

http://www.necta.go.tz/matokeo2014/ACSEE.htm

NDEGE YA NCHI MALASYIA YAUA 295 UKRAINE

NDEGE YA NCHI MALASYIA YAUA 295 UKRAINE

Miili ya watu imetapakaa kila upande katika kile kinachoaminika kuwa masalia ya ndege hiyo ya muundo wa jet karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga,.

Rais wa Ukraine alielezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua. .Ndege hiyo nambari MH17 ilikua inakaribia kuingia anga ya Urusi mawasiliano yalipokatizwa.
Inaaminiwa waasi hao wanaotaka kujitenga walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.
Anga ya Ukraine haikufungwa rasmi lakini mashirika ya ndege ya Ujerumani, Lufthansa, Air France ya Ufaransa na Uturuki,yanaliepuka eneo la Ukraine Mashariki.KWA MSAADA WA BBC SWAHILI

Thursday, 17 July 2014

VAN GAAL ATUA MANCHESTER UNITED KWA NDEGE BINAFSI

VAN GAAL ATUA MANCHESTER  UNITED KWA NDEGE BINAFSI

Huku ushabiki na mbwembwe za kombe la dunia zikibaki kumbukumbu,ushabiki sasa unarudi vilabuni, wana- Manchester United, wanamwangalia kwa karibu kocha wao mpya Louis van Gaal, amekuja na miujiza gani?
Alipowasili kwenye uwanja wa mazoezi Carrington amesema hana jipya zaidi ya kujenga mshikamano zaidi miongoni mwa wachezaji.
'Ni lazima tuimbe wimbo huohuo ulioisaida timu ya Uholanzi ililowaezesha kukaribia ushindi wa kombe la dunia na kuibuka nafasi ya tatu kwa kuwafunga wenyeji Brazil' amesiitiza
Lakini ufafanuzi zaidi ataotoa katika mkutano na waandishi habari baadae leo.
Kikosi hicho cha Man United kikiwa na wachezaji wapya akina Herrera na Luke Shaw, waliopatikana kwa gharama ya zaidi ya £millioni 56m,wataelekea Marekani ijumaa kwa ziara na kucheza angalau mechi tano.KWA MSAADA WA BBC SWAHILI

RAISI GOODLUCK JONATHAN AOMBA MSAADA DHIDI YA BOKO HARAMU

RAISI GOODLUCK JONATHAN AOMBA MSAADA DHIDI YA BOKO HARAMU

Rais Goodluck Jonathan ametuma barua katika bunge la seneti ili kuidhinisha ombi hilo ambalo litasaidia kuimarisha vifaa vya kijeshi.

Huku umwagikaji wa damu ukiendelea Kazkazini mwa Nigeria ,rais Goodluck Johanathan anaendelea kupata shinikizo.Zaidi ya watu 2000 wameuawa mwaka huu katika ghasia zilizosababishwa na wapiganaji wa Boko haram.
Kuna ripoti kwamba wanajeshi wengi katika vita vya kukabiliana na wanamgambo hao hawana vifaa vya kutosha na hivyo basi kushindwa kuwakabili waasi hao.
Ijapokuwa jeshi halijakiri kuhusu madai hayo linakubali kwamba linahitaji vifaa zaidi ili kukabiliana na vita hivyo.
Rais Goodluck Johnathan anasema kuwa kuna umuhimu wa kulinunulia jeshi vifaa zaidi ili kukabiliana na tishio la Boko Haram.
Wakosoaji hatahivyo wamelishtumu jeshi kwa utumizi mbaya wa raslimali zilizopo.
KWA MSAADA WA BBC SWAHILI
MSHUKIWA WA UGAIDI TANZANIA AKAMATWA

Mshukiwa huyo amesomewa mashtaka ya kufadhili vitendo vya kigaidi nchini Kenya.nazohusiana
Pamoja naye watuhumiwa wengine 16 ambao wanadaiwa kuendesha vitendo vya kigaidi nchini Tanzania pia wamefikishwa mahakamani hii leo wakikabiliwa na tuhuma za kula njama ya kutenda makosa ya kigaidi nchini Tanzania.
Washtakiwa wote 17 wamerejeshwa rumande baada ya kusomewa mashtaka ya vitendo vya kigadi nchini Tanzania pamoja na nchi jirani ya Kenya.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali mwandamizi Prosper Mwangamila ulidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kuwa kwa kutumia mtandao wa facebook aliweza kushawishi watu wengine kuwasiliana kwa lengo la kutafuta vifaa vya kulipua mabomu nchini Kenya na kusababisha majerahi, hofu na Vifo.
Jihand Gaibon Swaleh ambaye amesomewa mashtaka mawili hakuruhusiwa kukiri wala kukana mashitaka yanayomkabili kutokana na kwamba mashitaka hayo yanaangukia katika makosa ya ugaidi ambayo kwa mujibu wa sheria nchini Tanzania mahakama ya Hakimu Mkazi haina mamlaka ya kuendesha kesi za namna hiyo.
Katika kesi ya awali kutajwa mahakamani hapo washtakiwa wengine 16 walisomewa mashtaka mawili ikiwemo kula njama kutenda kosa pamoja na kushawishi wenzao kushiriki katika vitendo vya kigaidi katika sehemu mbali mbali nchini Tanzania.
Ni makosa ambayo wanadaiwa kutenda kati ya Januari mwaka 2013 na Juni 2014 katika maeneo tofauti Tanzania.
Katika kesi zote mbili dhidi ya washtakiwa hao Upande wa mashtaka uliiambia mahakama iliyokuwa chini ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo bi Hellen Riwa kuwa upelelezi bado unaendelea na hivyo kuiomba mahakama kuahirisha kesi hizo hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Julai.
Awali mapema asubuhi msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania Bi Advera John Bulimba aliwealeza waandishi wa habari kuhusu tuhuma dhidi ya washtakiwa hao
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi kubwa la watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa pamoja wakikabiliwa na tuhuma za makosa ya kigaidi huku mtandao wa kijamii wa facebook nao ukitajwa kuhusika katika kutawanya taarifa za kuwezesha kutenda makosa hayo.KWA MSAADA WA BBC SWAHILI